CCM YAIGALAGAZA CHADEMA KWENYE DRAFT
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Wakati jana kukipigwa pambano la watani wa jadi wa soka la Tanzania Bara Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwania Ngao ya Jamii, maeneo ya Tabata pia Dar es Salaam kulipigwa mechi ya mchezo wa draft kati ya Steven Mruge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Thadeo Kirufi "Ted" wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika mchezo huo Steven Mruge wa CCM alimshinda Ted wa CHADEMA kwa mabao 3-2, washindani hao wawili walianza kwa kupaniana kabla ya kuanza kuchuana na walipoanza kucheza Mruge alikuwa akimnyanyasa Ted na kumfunga mabao hayo matatu.
Ingwe ya pili Ted alicharuka na kuanza kukomboa mabao hayo lakini mwisho mchezo huo ukawa umemalizika hasa baada ya kuanza kwa penalti Uwanja wa Taifa mchezo wa Simba na Yanga, Wakati huo huo ile michuano ya draft kuwania mchele kilo kumi itaendelea tena mwishoni mwa wiki kwa mechi nne za hatua ya robo fainali