Mwinyi Haji aitumia Simba salamu
Na Ikram Khamees. Pemba
Bao pekee lililofungwa kipindi cha kwanza na beki wa upande wa kushoto Mwinyi Haji Mngwali, limeipa ushindi wa bao 1-0 Yanga SC dhidi ya Jamhuri ya Pemba katika uwanja wa Gombani mjini hapa.
Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina alilazimika kupanga vikosi viwili ili kutesti silaha zake vizuri kabla ya Jumatano ijayo kumenyana na watani wao wa jadi Simba katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Huo ni ushindi wa pili mfululizo lakini ni wa tatu kwao tangu watue visiwani Zanzibar, Yanga iliifunga Mlandege mabao 2-0, Chipukizi 1-0 na Jamhuri pia kwa bao hilo, Simba nao jana waliichapa timu ya Gulioni mabao 5-0