KMC YAMWEKEA NGUMU RONALDO, MBEYA CITY
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Timu ya KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambayo inashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara imemwekea pingamizi kiungo wake Iddi Seleman maarufu Ronaldo ambaye amesajiliwa na Mbeya City.
Uongozi wa KMC umesema hautakubali kuona nyota wao anaichezea Mbeya City pasipo wao kulipwa chao, Mbeya City imekiuka taratibu kwa kumpa kandarasi mchezaji wao bila kuwasiliana nao.
Ronaldo ni mchezaji wa KMC na bado ana mkataba na timu hiyo hivyo Mbeya City ya mkoani Mbeya ilipaswa kuwafuata, kwa sasa KMC wanataka walipwe chao ama sivyo mchezaji huyo hatoichezea timu hiyo msimu ujao