Kesho ni Simba na Ruvu Shooting Taifa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajia kuanza rasmi kesho ambapo viwanja saba vinatatimua vumbi kwa timu 14 kushuka uwanjani.
Lakini mechi ambayo itakuwa balaa ni kati ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tayari vijana wa Ruvu Shooting wanaotokea kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu Mlandizi mkoani Pwani wapo Dar es Salaam kujiandaa na mchezo huo.
Simba ambao wametoka kutwaa Ngao ya Jamii Jumatano iliyopita baada ya kumfunga mtani wao wa jadi Yanga mabao 5-4 kwa changamoto ya penalti baada ya sare tasa 0-0 Uwanja wa Taifa, wapo kamili kuwavaa wanajeshi hao na Msemaji wa Simba Haji Sunday Manara amesema ushindi kwao ni kama uji kwa mgonjwa.
Lakini msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amejinadi kuibuka na ushindi kwa kudai Simba ni sawa na toi la Kichina kwani Kariakoo hakuna Simba