Tff yaishitukia Kagera Sugar kwa Mbaraka Yusuf
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (Tff) limeishitukia klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera juu ya kumwekea pingamizi mchezaji mpya wa Azam FC, Mbaraka Yusuf ikisema ni mali yao na Azam FC walikiuka taratibu kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Katika malalamiko yao Kagera Sugar walidai Mbaraka Yusuf wana mkataba nae wa miaka mitatu na alitumikia miaka miwili hivyo bado ni wao na Azam walitakiwa wawafuate ili kutamgaza ofa ya kumuhitaji lakini hawakufanya hivyo.
Azam nao wamesema wao wamemsajili kihalali Mbaraka kwani mkataba wake na Kagera ulikuwa umemalizika na ndio maana wakampa mkataba wa miaka miwili, Lakini nao Tff kupitia kwa Afisa Habari wake Alfred Lucas ameshangazwa na madai ya Kagera Sugar dhidi ya Azam kuhusu mchezaji Mbaraka Yusuf.
Lucas amesema kama Kagera inasema ukweli kuwa Mbaraka ni mali yao mbona hawakumuorodhesha katika kikosi chao cha msimu ujao na hofu ya Tff kwamba endapo Kagera itashinda kesi yake hiyo ina maana Mbaraka hatocheza ligi hivyo Kagera anahisi ni wababaishaji na Azam wako sahihi