MO AWEKEWA KAUZIBE SIMBA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kuna uwezekano mkubwa mfanyabiashara kijana barani Afrika, Mohamed Dewji "Mo" akashindwa kuwekeza bilioni 20 yake katika klabu ya Simba kwa lengo la kununua Asilimia 51 ya Hisa baada ya klabu hiyo kuja na mkakati mpya wa masharti ya wawekezaji.
Mmoja kati ya viongozi wa Simba waliopewa dhamana ya kuipeleka klabu hiyo kuwa kampuni, Mulamu Ng' ambi amesema ni marufuku kwa mwanachama yeyote wa Simba kununua Hisa zaidi ya 50 katika klabu hiyo.
Akizungumza leo Ng' ambi amesema wamekubaliana kuwa endapo hisa zitaanza kuuzwa basi mwisho wa kumiliki ni 50 ili kusiwe na mtu mwenye kumzidi mwenzake kati ya klabu na mwekezaji, pia amesema klabu ndiyo itakayokuwa na kauli tofauti na mwanzo ambapo ilisemekana kuwa kama bilionea Mo Dewji angeinunua Simba kwa bilioni 20 angekuwa na kauli ya mwisho.
Lakini sasa hata kama Mo Dewji atainunua Simba bado atabaki kama mwanachama wa kawaida na wala hatokuwa na sauti, hii ni sawa na kuwekewa kauzibe na kuna uwezekano akashindwa kuwekeza