Simba yawasili Dar kuiwahi Yanga
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Simba SC mchana wa leo imewasili ikitokea Zanzibar ambapo ilikwenda kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na pambano lake la Jumatano ijayo na mtani wake wa jadi Yanga SC katika uwanja wa Taifa kuwania Ngao ya Jamii.
Simba ilikaa Unguja ambapo pia ilicheza mechi mbili za kirafiki, Wekundu hao wa Msimbazi walicheza na Mlandege katika uwanja wa Amaan na kulazimishwa sare tasa 0-0 kisha ikaiduwaza Gulioni mabao 5-0.
Kocha wa Simba, Mcameroon Joseph Omog amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wao na Yanga na wamemuahidi ushindi, Yanga nao wapo Zanzibar katika kisiwa cha Pemba ambapo nao walicheza mechi mbili ingawa walicheza tatu ikiwemo moja waliyoicheza Unguja na Mlandege na kushinda 2-0, mechi nyingine Yanga ilizifunga Chipukizi na Jamhuri zote bao 1-0