Simba wapo tayari kuiua Yanga kesho
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Homa ya mpambano wa watani wa jadi kesho kati ya Simba na Yanga imezidi kupanda ambapo kila timu ikiwa imejiandaa kumkabili mwenzie, Simba leo wamemaliza mazoezi yao kabla jioni ya kesho hawajaivaa Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kocha mkuu wa kikosi hicho Mcameroon Joseph Omog amesema kikosi chake kipo tayari kwa vita hiyo ila amewaambia mashabiki wa Simba, kwamba kesho Yanga anakufa atake asitake.
Kiungo mwenye udambwidambwi mwingi, Mnyarwanda Haruna Niyonzima ametamba kuwalaza mapema mashabiki wa Yanga, amesema mashabiki wa Simba wajitokeze kushuhudia kalamu ya mabao wakiwafunga Yanga ambao aliwahi kuwatumikia.
Simba ilirejea juzi ikitokea Zanzibar ambako iliweka kambi yake kujiandaa na mchezo huo, Yanga nao walikuwa Pemba ambapo inasemekana wametua leo