Fifa yaipongeza Tff kwa kupata uongozi mpya
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Shirikisho la soka duniani,(Fifa) limewapongeza viongozi wote wapya waliochaguliwa kuliongoza tena kwa miaka minne ijayo.
Fifa kupitia kwa rais wake, Gian Ifontinho amewatumia salamu za pongezi viongozi hao ambao walishinda katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma.
Wallace Karia alichaguliwa kuwa rais wa shirikisho hilo wakati Michael Wambura alichaguliwa kuwa makamu wa rais huku wajumbe wa kamati ya utendaji nao wakiingia katika shirikisho hilo.
Uongozi wa Jamal Malinzi ulimaliza muda wake lakini ukashindwa kusimama imara baada ya Malinzj na watendaji wake kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa kukutwa na makosa mbalimbali ikjwemo kughushi nyaraka na utakatishaji fedha