Simba kuendeleza mauaji kwa Ruvu Shooting leo!

Na Saida Salum. Dar es Salaam

Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC jioni ya leo inashuka katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuchuana na masarange wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara..

Simba ambao Jumatano iliyopita iliifunga Yanga mabao 5-4 kwa changamoto ya penalti, baada ya kutoka sare tasa 0-0 ndani ya dakika 90 na kutwaa Ngao ya Jamii, leo itataka kuendeleza mauaji ili kuzidi kuwafurahisha mashabiki wake.

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara amesema ni lazima Simba leo ishinde kwakuwa wanataka kuwathibitishia mashabiki wake kuwa msimu huu watabeba ubingwa wa VPL.

"Mashabiki njooni kwa wingi uwanjani mushuhudie kikosi chenu kinavyoanza ligi kwa kishindo na msimu tutabeba ubingwa", alisema Manara ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara "Computer"

Wachezaji wa Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA