Stars yaitwanga Burundi 2-1, Mavugo aendelea kumtungua Dida
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imefanikiwa kuitwanga Burundi mabao 2-1 mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Huu ni mchezo wa pili mfululizo Stars ikipata ushindi, Jumamosi ya juma lililopita Stars iliilaza Botswana mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa, Stars inayonolewa na Salum Mayanga inaonekana kuimarika na kutia matumaini. Ilijipatia bao la kuongoza lililofungwa na winga Simon Happygod Msuva, hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa bao hilo, Burundi ilisawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake Laudit Mavugo ambaye anaichezea Simba ya Tanzania. Bao hilo la Mavugo ni kama mwendelezo wake wa kumtungua kipa Deogratus Munishi "Dida" anayeichezea Yanga pia ya Tanzania, bao la pili na la ushindi la Stars lilifungwa na Mbaraka Yusuph