Simba waitisha Madini, wapiga tizi kali

Na David Pasko. Arusha

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba SC kimetua salama jijini Arusha jana na kupata mapokezi makubwa ambapo mashabiki wengi walijitokeza kwenda kuilaki, na jana hiyo hiyo walianza mazoezi mepesi na leo wakaendelea kupiga tizi.

Simba SC watashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta kuchuana na Madini FC ya hapa Arusha mchezo wa Robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup, mechi itachezwa Jumamosi.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Hiliki "Kaburu" amesema kikosi chake kimepania kupata ushindi katika mchezo huo kwani sasa hawataidharau timu yoyote watakayokutana nayo hasa kwa zile zinazozaniwa ni ndogo.

"Kwenye Football hakuna timu ndogo wala changa, timu zote ni sawa isipokuwa kuna zile zenye mashabiki wengi na zisizo na mashabiki, ila Madini hatutaidharau kwani imeweza kuingia hatua kubwa kama hii, tutawapiga kama Polisi Dodoma". Alisema Kaburu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA