Yanga yaitumia salamu Zanaco, yaisurubu Kiluvya United 6-1

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Yanga SC imefanikiwa kuingia robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup kwa uahindi mnono wa mabao 6-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam dhidi ya Kiluvya United ya Dar es Salaam mchezo wa kukamilisha hatua ya 16.

Katika mchezo huo wa upande mmoja, Yanga iliandika mabao yake kupitia kwa mshambuliaji wake Mzambia Obrey Chirwa aliyefunga magoli manne peke yake na kuvunja rekodi ya Mrundi Amissi Tambwe aliyewahi kufunga magoli manne.

Magoli mengine yalifungwa na Geofrey Mwashiuya na Juma Mahadhi wakati lile la Kiluvya United lilifungwa na Edgar Charles baada ya kumtambuka beki wa Yanga Mtogo Vincent Bossou, kwa ushindi huo Yanga itakutana na Tanzania Prisons hatua ya robo fainali katika uwanja wa Taifa.

Pia ushindi huo ni salamu kwa wapinzani wao Zanaco ya Zambia ambao watakutana nao Jumapili mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika raundi ya kwanza, mechi hiyo itapigwa Jumapili ijayo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA