Simba yaifuata Mbao nusu fainali

Na David Pasko. Arusha

Goli lililofungwa katika kipindi cha pili na mshambuliaji wa kimataifa raia wa Burundi Laudit Mavugo limeipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Madini FC ya Arusha na kufanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup.

Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta ikiudhuriwa na maelfu ya watazamaji waliotokea mikoa jirani ikiwemo Dar es Salaam.

Vijana wa Madini walucheza vizuri na kuelewana vema na kufanikiwa kuidhibiti Simba katika kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana, kipindi cha pili Simba iliamua kufanya mabadiliko ambayo yalileta nguvu mpya na kupata bao la ushindi.

Simba sasa imeingia nusu fainali na inakuwa timu ya pili kufanya hivyo kwani jana timu ya Mbao FC iliingia nusu fainali baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1, Yanga itacheza na Prisons hatua ya robo fainali ili kuungana na Mbao na Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA