YANGA, ZANACO HAKUNA MBABE
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Yanga SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanamaanisha Yanga watahitaji ushindi wa ugenini katika mchezo wa marudiano nchini Zambia ili kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa kutoka Djibout, Djamal Aden Abdi aliyesaidiwa na Hassan Yacin na Farhan Salime hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na winga machachari wa timu hiyo Simon Msuva dakika ya 39 baada ya kuwachambua mabeki wa Zanaco kufuatia pasi nzuri ya kiungo Mzambia Justin Zulu.
Bao hilo lilikuja baada ya Yanga kubadilisha maarifa ya kuwashambulia Zanaco, kutokea pembeni hadi kuamua kuingia ndani ya eneo la hatari kwa kugongeana pasi. Kwa dakika zote 30 za awali.
Zanaco wakafanikiwa kukomboa bao katika dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana, Attram Kwame aliyetumia mwanya wa mabeki wa Yanga waliozubaa kusubiri wapinzani wao watoe nje mpira kiungwana (Fair play) baada ya mchezaji mwenzao Obrey Chirwa kuangushwa