Yanga kujiuliza kwa Kiluvya United
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara na mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la TFF Yanga SC wanashuka dimbani kuwavaa Kiluvya United katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo huo wa robo fainali ya kombe la Azam unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua hasa kutokana na Kiluvya United kutaka kuikamia zaidi Yanga ambao ni miamba ya soka nchini.
Mechi hiyo inachezwa Jumanne na Katibu mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema mchezo utakuwa mgumu kwakuwa wapinzani wao hawatakubali kupoteza, "Timu ndogo zinapokutana na timu kubwa huwa shughuri pevu kwani zinakamia sana", alisema Mkwasa ambaye kitaaluma ni kocha