HASSAN KABUNDA MCHEZAJI BORA VPL FEBRUALI
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa Mwadui FV ya Shinyanga, Hassan Salum Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Februali mwaka huu.
Kabunda ambaye ni mtoto wa beki wa zamani wa Yanga SC, Salum Kabunda "Ninja" au Msudan anechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwezi Februali baada ya kuwashinda Mrundi Laudit Mavugo na mzalendo Ibrahim Ajibu wote wa Simba.
Kabunda ameisaidia Mwadui kushinda mechi mbili mfululizo huku yeye akifunga mabao manne katika mechi tatu alizocheza kwa mwezi huo Februali, kiungo ambaye jana alijumuhishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars na kocha mzalendo Salum Mayanga.
Kabunda sasa atakabidhiwa kitita cha shilingi Milioni moja na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas ndiye aliyetoa taarifa hizi kupitia mahojiano yake na waandishi wa habari leo