Azam FC sasa kugeukia kimataifa
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC sasa inageukia anga za kimataifa baada ya usiku wa kuamkia jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex uliopo Chamazi.
Kikosi hicho kitashuka dimbani Machi 12 katika uwanja wao wa Azam Complex kuchuana na wageni wao Mbabane Swallors ya Swaziland mchezo wa raundi ya kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mtendaji mkuu wa Azam Saad Kawemba ameiambia Mambo Uwanjani leo kuwa Azam iko kamili kwa kuliwakilisha vema taifa na itafanya kweli katika michuano hiyo inayoshika nafasi ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa upande aa vilabu