Banda mchezaji bora Simba
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kiungo Abdi Hassan Banda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Klabu ya Simba wa mwezi Februali.
Banda ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza tangu arejee kwenye kikosi cha kwanza, kiungo huyo mrefu anayemudu kucheza nafasi zote za ulinzi amecheza vizuri mwezi Februali na kuiwezesha klabu hiyo kuendelea kukaa kileleni.
Kwa maana hiyo Banda atazawadiwa kitita cha shilingi Laki tano za Kitanzania ambazo hutolewa kwa mchezaji bora wa mwezi, Banda ameshinda tuzo hiyo wakati Laudit Mavugo alishinda pia tuzo kama hiyo Januari