Samatta aing' arisha Stars, apiga zote mbili
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa na nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jioni ya leo ameing' arisha Taifa Stars baada ya kuifungia goli moja kila kipindi na kuifanya Stars iibuke na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Botswana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Huo ni ushindi wa kwanza kwa kocha mzalendo Salum Mayanga aliyerithi mikoba ya mzalendo mwenzake Charles Boniface Mkwasa, Samatta aliifungia Stars bao la mapema la kuongoza katika kipindi cha kwanza.
Nahodha huyo leo aling' ara vilivyo akicheza vizuri licha ya kukosa mtu wa kuelewana naye kwani Stars ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa zaidi, Samatta alifunga bao la pili na la ushindi.
Baada ya mchezo wa leo, Stars sasa inajiandaa kwa mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Burundi, katika mchezo wa leo winga Simon Msuva alipoteza nafasi nyingi za wazi