Simba waapa kuifanyia mauaji Polisi Dodoma leo
Na Saida Salum. Dodoma
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Simba SC jioni ya leo nao wanajitupa katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa kucheza na timu ya maafande wa Polisi Dodoma mchezo wa kirafiki.
Simba ambao waliwasili jana na kupokewa na maelfu ya wapenzi wa soka mjini hapa, walialikwa na chama cha soka mkoa Dodoma (DOREFA) wanacheza na Polisi Dodoma ambao wanashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara.
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara amesema kikosi chake kimepania kuendeleza wimbi la ushindi bila kuangalia wanakutana na timu gani, Manara amedai Simba na Polisi Dodoma zimekuwa zikikamiana sana hasa zilipokuwa zinakutana kwenye Ligi Kuu Bara.
Simba ipo Dodoma ikiwa njiani kuelekea Arusha ambapo mwishoni mwa wiki ijayo itacheza na Madini ya Arusha mchezo wa Robo fainali kombe la TFF