Nay wa Mitego akamatwa na polisi
Na Ikram Khamees. Morogoro
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibarik maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na jeshi la polisi mjini hapa akiwa kwenye shoo zake za kimuziki.
Taarifa iliyopatikana inasema Nay wa Mitego amekamatwa na polisi Mvomero lakini bado haijawekwa wazi kipi kilichopelekea kukamatwa kwake.
Lakini chanzo chetu kimabaini kuwa msanii huyo amekamatwa na polisi kwa sababu ya kuachia wimbo wake mpya uitwao 'Wapo' ambao ndani yake una maneno yenye ukakasi, wimbo huo umemdisi waziwazi rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ukimwambia kuwa amezuia uhuru wa habari na serikali yake inaendeshwa kwa kiki