Bocco apelekwa Afrika Kusini
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Nahodha na mshambuliaji wa Azam FC John Bocco "Adebayor" anapelekwa nchini Afrika Kusini kutibiwa goti linalomsumbua kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC.
Bocco aliumia katika mchezo huo licha ya Azam kushinda bao 1-0 goli ambalo lilifungwa naye, Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema Bocco atapelekwa Afrika Kusini kufanyiwa matibabu.
Maganga pia amesema mbali na Bocco, Azam ina majeruhi wengine ambao ni Agrey Morris na Mcameroon Stephen Kingue, Azam imetolewa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuchapwa jumla ya mabao 3-1