Mwanjali bado bado sana kurejea uwanjani
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Simba SC bado itaendelea kumkosa mlinzi wake wa kati Mzimbabwe Method Mwanjali aliyeumia hivi karibuni na kukosa mechi kadhaa za mashindano.
Daktari wa Simba Yassin Gembe amesema mchezaji huyo anaweza kurejea uwanjani mwezi ujao na sasa tayari ameanza mazoezi mepesi mepesi ingawa bado hali yake haijatengamaa.
Kukosekana kwa Mwanjali kumeweza kusababisha ukuta wa Simba kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara kwa mara, Mwanjali amesababisha pengo kubwa kwenye safu ya ulinzi ya Simba ambayo imeruhusu mabao manne ikicheza mechi kadhaa za Ligi Kuu ya Bara na kombe la TFF