MKWASA AAPA KUWABAKISHA NGOMA, BOSSOU
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Yanga SC kesho inatupa karata yake nyingine ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kombe la TFF itakapocheza na Kiluvya United mchezo wa robo fainali Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ameanza kwa kuwaomba radhi mashabiki na wapenzi wa Yanga hasa baada ya kikosi chao jana kulazimishwa sare na Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mchezo huo ulifanyika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, lakini Mkwasa akatumia nafasi hiyo kuwaambia Wanayanga kuwa licha kwamba wanapitia msoto mkali lakini anajotahidi angalau kuwabakisha mastaa wote wa kikosi cha kwanza wanaomaljza mikataba yao.
Mkwasa amesema atawabakisha Donald Ngoma, Thaban Kamusoko raia wa Zimbabwe ambao mikataba yao inamalizika, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, Amissi Tambwe Burundi na Vincent Bossou raia wa Togo, nyota hao wote wataendelea kukipiga Yanga alisema Mkwasa ambaye amewahi kuichezea timu hiyo na baadaye kuwa kocha kwa vipindi tofauti