Yanga kuanza kwa mashambulizi
Na Msham Hassan. LUSAKA
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Dar Young Africans maarufu Yanga SC jioni ya leo inashuka Uwanja wa Mashujaa mjini Lusaka kurudiana na Zanaco mchezo wa hatua ya 32 bora ya Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Katika mchezo huo Yanga itaanza kwa kushambulia mwanzo mwisho ili angalau kupata bao la ugenini na ikiwezekana kushinda mchezo huo, katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam, Zanaco iliilazimisha sare ya kufungana 1-1 Yanga.
Hivyo katika mchezo wa leo Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote kitendo ambacho kinaifanya mechi hiyo ionekane kali na ya kusisimua, Yanga huenda ikaanza na Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa ambao watacheza kwa kushambulia zaidi ingawa wapinzani wao wanaonekana ni wazuri mno wakiwa nyumbani