Nay wa Mitego asema hakuna wa kumzuia asianzishe kanisa lake
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Emmanuel Elibarik maarufu Nay wa Mitego amesema hakuna mtu yeyote wa kumzuia asianzishe kanisa lake la uponyaji mara tu atakapoamua kufanya hivyo.
Nay wa Mitego amesema Mzee wa Upako hawezi kumzuia adianzishe kanisa kwakuwa hata yeye ameanzisha kanisa na hakukuwa na mtu wa kumzuia.
Msanii huyo amepanga kuanzisha kanisa mara baada ya kuachana na muziki, "Kwa sasa bado nafanya muziki wa kidunia, ila nitakapoona inatosha basi nitafungua kanisa langu na kumtumikia Mungu", msanii huyo anayetamba na wimbo wa "Muda wetu".
Hivi karibuni Mzee wa Upako alisema endapo Nay ataanzisha kanisa lake basi atamshitaki, lakini Nay amemjibu kwakusema hakuna mtu mwenye uwezo wa kumzuia asifungue kanisa lake