Kagera Sugar wasema wataisimamisha Simba

Na Mwandishi Wetu. Bukoba

Kocha mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime amesema kikosi chake hakitakubali kugeuzwa ngazi ya kuelekea kwenye ubingwa na Wekundu wa Msimbazi Simba SC watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mexime ameyasema hayo mapema kuelekea katika mchezo huo ambao utapigwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Mexime amedai anaifahamu vizuri Simba na hatishwi na soka lao hivyo amewataka wapenzi na mashabiki wa Kagera Sugar kuwa na uhakika wa ushindi.

Mexime amedai Kagera Sugar inataka kumaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu hivyo ni lazima washinde mechi zao za mwisho hasa wanazochezea uwanja wa nyumbani, "Kwa sasa tunataka kukamata nafasi ya tatu, najua ukiwa mshindi wa tatu unapewa zawadi hivyo tuna uhakika mkubwa wa kuchukua kitita cha wadhamini", amesema Mexime, Simba na Kagera Sugar zitakutana hivi karibuni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA