CONTE AWATAKA CHELSEA KUTOBWETEKA
Mkufunzi mkuu wa Chelsea ya England Antoine Conte amewataka wachezaji wake kutobweteka na matokeo na badala yake kukaza kila wabapokutana na timu pinzani licha kwamba wako kileleni kwa uwiano wa pointi 10 na washindani wao wakuu kwenye mbio hizo Tottenham Hotspur.
Chelsea waliifunga West Ham mabao 2-1 lakini amegundua kuwepo ushindani mkubwa kwa kila timu inayokutana nayo, amedai vilabu hukamia mno ili kuwashinda lakini amewataka vijana wake kupambana hadi tone la mwisho kwani wakibweteka wanaweza kupokwa uongozi.
Mkufunzi huyo anaamini kupambana kwa vijana wake kutawafanya waendelee kuwa kileleni kwani hadi sasa wanaongoza kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya wapinzani wao Tottenham Hotspur