Jeuri ya Manji kurejea upya Jangwani
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Baada ya Mahakama kuu ya Tanzania kumrejesha uraiani mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji na kutakiwa kuendelea na shughuri zake za kawaida, imebainika kuwa kibopa huyo wa Quality Group anarejesha tena jeuri Jangwani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimesema kwa sasa Manji bado mgonjwa na anaendelea na matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam lakini bosi huyo amepanga kumwaga noti za maana Jangwani ili kurudisha morali kwa wachezaji.
Manji ameumizwa sana na suala la kuhusishwa na matumizi ya unga na alikasirishwa zaidi kwa kitendo cha kuendelea kushikiliwa na serikali muda wote mpaka pale mahakama ilipotoa mwongozo kuwa yuko huru na hapaswi kushikiliwa.
Akaunti za kibopa huyo zimeachiwa ina maana fedha sasa zitaanza kumiminika Jangwani kama ilivyokuwa nyuma, Manji anataka kuona ubingwa wa bara unaendelea kubaki Jangwani, kilisema chanzo hicho