Chacha, Matandika washinda kesi yao ya rushwa
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Maofisa wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) wameshinda kesi yao ya tuhuma za rushwa iliyokuwa ikiwakabili, Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa rais wa TFF Jamal Malinzi na Martin Chacha aliyekuwa mkurugenzi wao wa mashindano wa TFF walikuwa wanashutumiwa kuomba rushwa ya milioni 25 kwa viongozi wa Geita Gold Mine wameachiwa huru.
Sauti zilizodaiwa kuwa ni zao zilisikika zikieleza mipango ya kusaidia Geita Gold na ilitakiwa fedha kwa ajili pia ya kuwapa viongozi wengine.
Ingawa wadau wengi wanaojua sauti zao waliamini ni wao kabisa, lakini Mahakama ya Mkazi Kisutu imetupilia mbali ushahidi wa sauti uliowasilishwa mahakamani hapo