TRA yafunga ofisi za TFF kisa deni la mamilioni

Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam

Mamlaka ya kukusanya mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ikidai mamilioni ya shilingi yanayosemekana tangu enzi za utawala wa aliyekuwa Rais Leodegar Tenga na sasa Jamal Malinzi.

Madalali wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart walivamia ofisi za Tff na kuwatoa nje maofisa wote na wafanyakazi wa Tff nje ya ofisi hizo na kufunga, TRA inaidai TFF mamilioni ya shilingi ikidaiwa ni ya kodi.

Fedha hizo zinasemekana ni makato ya kodi za makocha wa timu ya taifa, Taifa Stars ikianzia na Mbrazil Marcio Maximo, Jan Poulsen, Kim Poulsen na Mart Nooij, kufungwa kwa ofisi hizo za Tff zinaweza kuathili soka la Tanzania

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA