Singida United yampa mikoba Pluijm naye aanza kazi rasmi
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam
Aliyekuwa kocha na mkurugenzi wa ufundi wa Yanga SC, Hans Van der Pluijm amejiunga na timu iliyopanda Ligi Kuu ya Singida United ya mkoani Singida ambayo inahudumiwa kwa ukaribu zaidi na Waziri wa mambo ya ndani Mhe Mwigulu Nchemba (MB).
Pluijm ameteuliwa kukinoa kikosi hicho kinachovaa uzi wa njano kama Yanga, ambapo pia ameanza kufanya usajili wa wachezaji akiwaandaa kwa msimu ujao, Singida United imepanda Ligi Kuu sambamba na Njombe Mji na Lipuli ya Iringa, kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili