YANGA NA WAARABU TENA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar Young Africans maarufu Yanga SC wamepangwa tena na timu za Afrika ya Kaskazini katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga imepangwa na Moulodia Club Alger ya Algeria katika mchujo wa kufuzu hatua ya makundi inayishirikisha timu 16, Yanga imejikuta ikiangukia michuano hiyo baada ya kutolewa kwenye Ligi ya mabingwa Afrika na Zanaco ya Zambia kwa goli la ugenini.
Yanga imekuwa na bahati mbaya hasa inapokutana na timu za Kiarabu na mara zote imekuwa ikitolewa, kwa maana hiyo Yanga inaweza kuishia hapo kwani matumaini finyu ya kuwang' oa Waarabu