Jerry Muro amtilia shaka Lwandamina
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga SC ambaye amesimamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jerry Colnery Muro amefunguka juu ya uwezo wa kocha Mzambia George Lwandamina.
Muro ambaye adhabu yake inamalizika Mei mwaka huu, amedai hakuna dhambi kubwa itakayowatafuna Wanayanga ni kuondoka kwa Mholanzi Hans Van der Pluijm aliyeipa mafanikio timu hiyo.
Msemaji huyo mwenye maneno ya kejeli hasa kwa mahasimu wao Simba, amedai kuna tofauti kubwa kati ya Hans na Lwandamina ambapo amedai Lwandamina ni kocha mzuri lakini hawezi kuisaidia Yanga kwa mfumo wake.
"Mfumo wa Lwandamina haueleweki kabisa, Yanga hawachezi, angalia timu imeshindwa kuzifunga Azam, Simba na Mtibwa ambazo ndio washindani wa Yanga, pia Yanga imeshindwa kwenye michuano ya kimataifa, Yanga itamkumbuka sana Hans", amesema Muro huku akichukizwa na matokeo mabaya ya timu