Rais Magufuli ampa tano Diamond Platinum
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli jana alimpigia simu mwanamuziki nyota nchini Naseeb Abdul "Diamond Platinumz" na kumpongeza alipokuwa live katika kipindi cha Tv Clouds.
Mheshimiwa rais Magufuli alilazimika kupiga simu na kumpongeza Diamond kutokana na jitihada zake kwenye muziki na kuitangaza Tanzania kimataifa, Magufuli amedai Diamond amekuwa balozi mzuri kwa taifa letu nje mipaka na atashikamana naye bega kwa bega.
Naye msanii Diamond amemuomba Rais Magufuli kuisaidia tasnia ya muziki ili waendelee na shughuri hiyo kwani imekuwa ikiwapatia kipato na kuendesha maisha yao ya kila siku, Diamond amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki na akishirikiana na wanamuziki wakubwa duniani