Yanga waondoshwa kwa bao la ugenini
Na Mshamu Hassan. Lusaka
Yanga SC imeondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kutoka sare ya 0-0 na wenyeji wao Zanaco mchezo wa marudiano uliopigwa katika uwanja wa Mashujaa.
Kwa maana hiyo Yanga inaangukia kombe la Shirikisho ikianzia kucheza mechi mbili kabla ya kufuzu hatua ya makundi inayoshirikisha timu 16.
Washambuliaji wa Yanga Simon Msuva na Obrey Chirwa walishindwa kuwatoka mabeki wa Zanaco ambao walikuwa wakiitafuta sare hiyo tasa ili wasonge mbele, Yanga inayonolewa na Mzambia George Lwandamina imeshindwa kuweka rekodi ya kuvuka makundi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Mholanzi Hans Van der Pluijm