AZAM FC MWENDO MDUNDO, YAIDUWAZA MBABANE 1-0

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika Azam FC wameanza vizuri michuano hiyo kwa kuichapa Mbabane Swallors ya Swaziland kwa bao 1-0.

Mechi hiyo ilipigwa kwenye uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam usiku, uliudhuriwa na mashabiki wengi waliotaka kuona Azam FC inamaliza kazi mapema.

Hata hivyo, Azam FC ililazimika kusubiri kwenye robo ya nne ya dakika 90 yaani dakika ya 25 za mwisho kupata bao dhidi ya Mbabane ambao walikomaa hadi mwisho wa dakika 45 mambo yakiwa 0-0.

Ushindi huo unailazimu Azam FC kuwa makini zaidi kulinda ushindi wake huo mfinyu itakapokuwa ugenini mjini Mbabane katika mechi ya pili itakayoamua matokeo.

Bao lililoipa ushindi Azam lilifungwa na winga machachari Ramadhan Singano "Messi" ambalo sasa litaifanya Mbabane kushinda mabao mawili itakaporudiana majuma mawili

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA