Zanaco waja kuendeleza ubabe kwa Yanga
Na Paskal Beatus. Dar es Salaam
Wawakilishi wa Zambia katika michuano ya Afrika, Zanaco imwasili nchini leo tayari kwa kibarua kizito dhidi ya wawakilishi wa Tanzania Yanga SC kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.
Mchezo wa raundi ya kwanza Ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga na Zanaco utachezwa mwishoni mwa wiki hii na tayari Zanaco wameshatua nchini kwa ajili ya mpambano huo, Hii ni mechi ya kisasi kwani mwaka 2006 Zanaco iliitoa Yanga katika michuano kama hiyo.
Yanga ilitolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam kulazimishwa sare ya 2-2 na kisha kulala 1-0 Zambia, hata hivyo mechi hiyo itakayopigwa uwanja wa Taifa itaonyeshwa Live na Azam TV na tayari Yanga imeshauza haki za matangazo