Muziki upo Taifa leo, Yanga vs Zanaco, Lwandamina aanza na Tambwe, Ngoma, Msuva na Chirwa
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara Dar Young Africans maarufu Yanga SC jioni ya leo inatelemka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwakaribisha majirani Zanaco ya Zambia mchezo wa hatia ya 32 Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Mabingwa hao wa Bara ambao kwa sasa wapo kwenye msoto wa fedha lakini wameahidi kupigana kufa au kupona ili kuweza kuchomoza na ushindi katika mchezo huo wa kwanza ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi, endapo Yanga itafuzu makundi itaweza kujipatia mamilioni ya shilingi kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo.
Mkufunzi mkuu wa Yanga Mzambia George Lwandamina amewaanzisha washambulizi wake hatari na tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Bara mara 26 na tumaini kubwa kwa mashabiki hao, Lwandamina amesndelea kumuamini kipa Deogratus Munisi Dida akinpanga langoni huku akisaidiwa na mabeki Hassan Kessy, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Vincent Bossou na Thabani Kamusoko.
Wengine Simon Msuva na Obrey Chirwa wakicheza kama viungo wa pembeni wakati Haruna Niyonzima akisimama katikati kama kiungo mchezeshaji huku Amissi Tambwe na Donald Ngoma wakisimama kama washambuliaji. Yanga inahitaji ushindi angalau wa magoli matatu kwa bila