Simba yapata mwaliko Dodoma

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC wamepata mwaliko maalum kutoka kwa chama cha soka mkoani Dodoma (DOREFA) na watacheza mechi ya kirafiki Jumamosi ijayo tarehe 11/3/2017.

Haji Sunday Manara ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo amesema klabu yake imealikwa na DOREFA kwa lengo la kwenda kuwasabahi wakazi wa Dodoma.

Manara amedai Simba ina mashabiki wengi Dodoma na kwa bahati mbaya mkoa huo hauna timu ya Ligi Kuu hivyo wamekosa kuona mechi zao kwa muda mrefu, Manara amesema Simba itacheza na Polisi Dodoma siku ya Jumamosi katika uwanja wa Jamhuri.

Wekundu hao ambao wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 55 itatumia ziara hiyo kujiweka sawa na ligi ambayo itasimama kwa wiki moja, Manara amedai Simba itasafiri na wachezaji wake wote

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA