Nape afunika Taifa, mashabiki waimba "Nape.....Nape....Nape

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilipocheza na Botswana mchezo wa kirafiki.

Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Nape Moses Nnauye alikuwa gumzo mara baada ya kuwasili uwanjani hapo kushuhudia mtanange huo.

Nape alizoa mashabiki lukuki ambao walimzonga huku wengine wakitaka kupiga naye picha, Waziri huyo aliyedumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye serikali ya JPM alikuwa kivutio kikubwa.

Baadaye Nape aliungana na waziri aliywmrithi kwenye wizara hiyo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe na kukaa naye jukwaa moja kisha baadaye meneja wa zamani wa Yanga, Mohamed Bhinda aliwafuata wote na kuwakumbatia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA