Azam FC yatupwa nje kombe la Shirikisho, yapigwa 3-0

Na Mrisho Hassan. Mbabane

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CC) Azam FC jioni ya leo imetupwa nje ya michuano hiyo baada ya kubutuliwa mabao 3-0 na wenyeji wao Mbabane Swallors ya Swaziland.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC itolewe kwa jumla ya mabao 3-1 kufuatia ushindi wa 1-0 ilioupata jijini Dar es Salaam, katika mchezo wa leo Azam walicheza vizuri na kwa maelewano lakini wakajikuta wakipotea mchezoni baada ya kufungwa bao la kwanza.

Mabingwa hao wa kombe la Mapinduzi sasa watahamishia nguvu zao kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya Azam Sports Federation Cup ambao wameingia robo fainali

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA