NGASA- NARUDI FANJA
Na Albert Babuu. Dar es Salaam
Kiungo mshambuliaji wa Mbeya City Mrisho Khalfan Ngasa amesema atarejea tena Oman kujiunga na klabu yake ya Fanya inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ngasa aliyejiunga na Fanja kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Free State Stars ya Afrika Kusini, aliamua kurejea nyumbani kujiunga na Mbeya City kufuatia kumalizika kwa pasipoti yake ya kusafiria ambapo ilimlazimu kurejea nchini ili kushughurikia tatizo hilo.
"Ni kweli narudi Fanja FC ya Oman, milango imekamilika na kinachosubiriwa ni kumalizika mkataba wangu mwishoni mwa msimu, nilisaini mkataba mfupi ili niweze kurejea Oman kwa sababu nilikuja nyumbani kushughurikia hati yangu ya kusafiria", alisema Ngasa.
Ngasa aliibukia kupitia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys mwaka 2004 baadaye akatamba na Toto Africans kabla hajasajiliwa na Kagera Sugar ambayo nayo ikampeleka Yanga SC, Ngasa aliuzwa kwa Azam FC ambayo nayo ikampeleka kwa mkopo Simba kabla hajarejea tena Yanga kisha kujiunga na Free State ya Afrika Kusini ambako alivunja mkataba na kujiunga na Mbeya City, hata hivyo anarejea tena Umangani