Sunche na Kapeto madansa waliotikisa

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Ni miongoni mwa madansa waliojipatia umaarufu mkubwa katika miaka ya 2000 hasa kutokana na aina ya mtindo waliouanzisha.

Sunche na Kapeto (Pichani) ndio ninaowazungumzia leo, nimewamisi sana, ni jamaa zangu wa karibu wote wawili.

Wenyewe wamenigeuza ndugu yao, mara nyingi nimekuwa nao karibu, walianza kucheza kwenye kumbi za starehe na wikiendi hufanya shoo ya nguvu, miaka iliyopita wakati tasnia hiyo ilipokuwa na mashindano yake kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa, madansa hao ndio walipoibukia.

Walishiriki mashindano hayo kwa kutumia majina ya Big Cut (Kapeto) ambaye ni Kurwa na Small Cut (Sunche) ambaye ni Dotto.

Walifanya vizuri ingawa hawakuwa kuwa mabingwa wa taifa, baadaye waliamua kuachana na majina hayo na kujiita Sunche na Kapeto, walijipatia umaarufu mkubwa.

Baada ya fani ya udansa ilipoanza kudorola, Sunche na Kapeto wakajiunga na Tanzania One Theatle (TOT) iliyokuwa ikiongozwa na marehemu John Komba, TOT Plus Band ilitamba mno hasa ikiwa na waimbaji nyota kama marehemu Ramadhan Masanja "Banzastone", Mhina Panduka na Ally Choki.

Sunche na Kapeto wakaihama TOT na kuamua kujitegemea wenyewe kimuziki, wakaanza kucheza shoo za mitaani, T.I.D akaamua kuwatumis kwenye muziki wake ambapo madansa hao walishiriki kwenye video, ndio wakawa madansa wa kwanza kusheki.

Ama kweli madansa hao wametuachia kitu ambacho kina manufaa kwa muziki wetu, majina yao halisi ni Hassan Abdul (Kapeto) na Hussein Abdul (Sunche) hawa jamaa ni wacheshi na pia ni wapole

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA