Blagnon arejea Simba baada ya kudunda Oman
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC raia wa Ivory Coast Fredrick Blagnon hatimaye amerejea kwenye Klabu yake ya Simba baada ya kukataliwa Fanja FC ya Oman aliyojiunga nayo kwa mkopo.
Taarifa zilizoifikia Mambo Uwanjani zinasema kuwa Blagnon amerejea Simba baada ya kushindwa kuwaridhisha Fanja ambao walimchukua kwa mkopo wa miezi sita.
"Ni kweli Blagnon amerejea Simba na ataungana na wenzake kumalizia mechi za msimu", ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na uongozi wa Simba