Simba yaua Polisi Dodoma 3-0
Na Saida Salum. Dodoma
Simba SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Polisi Dodoma uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo ameendelea kuwatesa makipa wa Tanzania baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo huo wa kirafiki jioni ya leo.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika Simba wakiwa mbele kwa bao moja, lakini kipindi cha pili wakaongeza mabao mawili kupitia kwa winga wake machachari Shiza Ramadhan Kichuya kwa penalti na mshambuliaji Juma Luizio Ndanda akafunga la tatu.