Zanzibar yapata uanachama Caf
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, Caf limeipa uanachama wa kudumu Zanzibar leo katika mkutano wake unaoendelea.
Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Alfred Lucas Mapunda amesema Zanzibar imepewa uanachama na Caf hivyo sasa Tanzania itawakilishwa na timu mbili za taifa katika michuano ya Afrika.
"Zanzibar itashiriki michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa wakubwa na pia kwa vijana, kwa maana hiyo uteuzi wa timu ya taifa, Taifa Stars itakayoshiriki michezo ya Afrika haitahusisha wachezaji wa Zanzibar", alisema Lucas.
Awali Zanzibar ilikuwa mwanachama wa muda wa Caf ambapo uliwezesha vilabu vyake kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika (Cal) na kombe la Shirikisho Afrika (CC)