Madini waapa kufa na Simba
Na David Pasko. Arusha
Kocha mkuu wa timu ya Madini FC, Abdallah Juma amesema vijana wake wako fiti kuikabili Simba na wameapa kufia uwanjani siku ya Jumamosi.
Simba inakutana na Madini mchezo wa robo fainali ya kombe la TFF maarufu Azam Sports Federation Cup, na Juma amedai vijana wake hawana mchecheto na wataendeleza kile walichokifanya kwa Panone, JKT Oljoro na JKT Ruvu.
Kikosi hicho cha Madini ambacho kinashiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara kimepania kushinda mchezo huo na kimedai Simba si tishio kwao ni timu ya kawaida kama zilivyo nyingine