Serengeti Boys wapangwa na Mali, Angola na Niger, Afcon
Na Mwandishi Wetu
Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 maarufu Serengeti Boys imepangwa kundi B katika fainali za mataifa ya Afrika KWA vijana wa umri huo yanayotarajia kuanza huko Gabon.
Serengeti Boys imeoangwa pamoja na Angola, Niger na Mali ambayo huenda isishiriki fainali hizo kwakuwa imefungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu Barani Afrika (CAF).
Kufungiwa kwa Mali kunaweza kuipa ahueni Serengeti Boys ambapo sasa itahitaji kushinda mechi zake mbili tu ili ijihakikishie kushiriki fainali za kombe la Dunia kwa vijana zitakazofanyika India baadaye